Monday, May 30, 2016

Chris Brown amuongeza Wizkid kwenye ‘One Hell of A Nite Tour’ Ulaya

Wizkid tayari anaishi ile ndoto ambayo wasanii wengi wa Afrika bado wanaiota. Kutoka kushirikishwa kwenye wimbo wa Drake ‘One Dance’ uliopo kwenye album Views na ulioshika namba moja kwenye chart za Billboard 100, hadi sasa kuongezwa kwenye orodha ya wasanii watakaomsindikiza Chris Brown kwenye ziara yake ya ‘One Hell of A Nite Tour’ barani Ulaya.
13248976_820765204721577_268213544_n
Taarifa hiyo ilitolewa na Chris Brown mwenyewe kwenye akaunti yake ya Instagram kabla ya Wizkid naye kuandika: 5th – 11th June I’ll be supporting my brother @chrisbrownofficial !! Get ur tickets!! #Onehellofanitetour Bringing the African wave!!”
Wizkid ana wimbo aliomshirikisha muimbaji huyo wa Marekani mwenye mashabiki wengi.
SOURCE: BONGO 5

Rama Dee: Namsupport Lady Jaydee sababu ni ‘strong’Nguli na mkongwe wa muziki wa R&B nchini Rama Dee ametoa sababu ya kuonesha ushirikiano mkubwa katika harakati za muimbaji Lady Laydee. 13269373_888557321256134_322576829_n
Rama Dee ni miongoni mwa wasanii waliomsindikiza Lady Jaydee kwenye show yake ya Naamka Concert Mlimani City jijini Dar es Salaam
Akizungumza na mtangazaji wa kipindi cha Ladha 3600 cha EFM, Jabir Saleh, Rama Dee alisema anaendelea kumsupport Jide sababu ni msanii anayepambana na yupo serious kuhakikisha anafanya kilicho bora zaidi ili kuilinda heshima yake katika muziki.
13259667_979440052175047_1181828343_n
Rama aliongeza kuwa Jide ameweka historia kubwa sana katika tamasha la Naamka Tena Concert lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City kwani ni mfano tosha kwa wasanii wengine ambao hawapo serious na game.
13249768_1086284351439475_1823378610_n
Hitmaker huyo wa Kipenda Roho kwa sasa yupo nyumbani na ametoa shukrani kwa mashabiki wake na kuwaahidi kuwa atawapa surprise kabla hajaondoka kurudi Australia ambako ndiko makazi yake yaliko kwa sasa.
Muimbaji huyo amemuoa raia wa nchini Australia na wana watoto wawili pamoja.
SOURCE:BONGO 5

Meneja wa Alikiba, Seven Mosha, afanunua nini kitakachokuwepo kwenye Alikiba TV

Wikiendi iliyomalizika, kampuni ya usimamizi inayofanya kazi naye, Rockstar4000 imetangaza kuingia naye ubia kwa kuanzisha kile kilichopewa jina ‘Alikiba TV.’
Kwa wengi taarifa hiyo iliyoandikwa kwa Kiingereza haijaeleweka vizuri na hivyo nimelazimika kumtafuta meneja wake, Seven Mosha kumuomba atupe ufafanuzi zaidi.
“Aikiba amezindua Alikiba TV ambayo ni content kuhusiana na kazi yake – matukio yote around him kikazi itakayokuwa inapatikana kwenye YouTube channel yake na pia itaanza kuoneshwa kwenye vituo mbalimbali tukianza na SoundCity,” Seven ameiambia Bongo5.
“Alikiba TV itakuwa chini ya mwavuli wa Rockstar Television,” ameongeza.
Kwa mujibu wa tangazo hilo zaidi ya Soundcity ya Nigeria, vituo vingine vya runinga duniani vitakavyoshirikiana naye kwenye mradi huo vitatangazwa. Kwa sasa mashabiki wameombwa kusubcribe kwenye channel yake ya Youtube ili kutopitwa na chochote.
Wiki mbili zilizopita Alikiba alisainishwa recording deal na label maarufu duniani, Sony Music. Kiba anayefanya vizuri na wimbo wake Aje, amekuwa msanii wa pili baada ya Davido kusainishwa kile wanachokiita ‘global deal’ na label hiyo iliyo nyumbani kwa wasanii wakubwa duniani.
SOURCE:BONGO 5

Noorah alikuwa mbele ya wakati, wakati umefika mbona tunajifanya hatumkumbuki?

Miaka minane iliyopita nilikutana na Haji Noorah Mwanza. Ilikuwa ni katika miaka yangu ya mwanzo mwanzo ya kama mtangazaji wa Radio Free Africa. Bado nilikuwa bwana mdogo kiumri na hata kwenye kazi hiyo ambayo mmoja wa walimu wangu wa chuoni Father Mfumbusa alikuwa akiidharau sana. ‘Kazi ya utangazaji redio ni ya ajabu sana, unajifungia kwenye kichumba unaongea peka yako,’ Mfumbusa alikuwa akisema mara kibao. image Ni kweli utangazaji ndivyo ulivyo lakini naapa nilipokuwa nikijifungua studio na kuanza kupiga mayowe peke yangu, nilijihisi kama dunia yote ni yangu. Niliipenda kazi ile na kwa wanaokumbuka masikio yao hayakuwadanganya jinsi nilivyosikika nikifurahia. Mwaka 2007/08 Noorah alikuja Mwanza na hicho kilikuwa ni kipindi ambacho ukiambiwa umtaje rapper mwenye swagga na style kali za kuchana, ulikuwa huachi kumtaja Ngwair na Noorah. Si ajabu hasa ukizingatia kuwa wote walikuwa members wa Chamber Squad aka East Zoo. Hivyo nakumbuka rafiki yangu Kidboy alimpeleka Noorah kwake kulipokuwa na studio za Tetemesha maeneo ya Kilimahewa. Kwenye gari ndogo tuliyokuwa tumepanda, kulikuwa kunachezwa wimbo wa msanii wa Canada mwenye asili ya Lebanon aliyetamba enzi hizo, Massari na wimbo wake Real Love. Noorah alikuwa akiuimba wimbo huo kwa kila mstari kama wake vile na kukibaini kipaji chake kingine cha kuimba. Kwangu mimi na uanagenzi niliokuwa nao ilikuwa ni siku ya dhahabu kupanda gari moja na rapper huyo wa Shy town aliyekuwa si wa kukutana naye hivi hivi miaka ile. Noorah alikuwa wa moto na hakuna rapper aliyekuwa na uandishi na style kama yake. Hilo lilimpelekea kujibatiza jina na Babastylez. Pamoja na kuanza kupata jina kupitia wimbo wake Vijimambo, umaarufu wa Noorah ulifika kileleni kupitia wimbo Ice Cream aliomshirikisha Sumalee na kutayarishwa na marehemu Roy kupitia G Records. Ice Cream ni wimbo mkali uliokamilika katika kila kitu huku ukijikuta ukidhania Noorah rapper aliyeingia studio straight kutoka mtoni. Wimbo huo ulikuwa miongoni mwa nyimbo za kwanza kwanza za Bongo Flava zilizokuwa na video kali. Mashairi yake aliyokuwa akiyanakshi kidogo na maneno ya Kiingereza yalimfanya Noorah arap katika mtindo uliokuwa mbele ya wakati huo. Ni rap ambayo leo hii akiingia studio na akarudia kile kile, bado tungeendelea kumwelewa na angeendena na maisha ya leo. Idea za Noorah zilikuwa pasua kichwa na kwa rapper wa kawaida asingeweza kuzifanikisha. Ngoma kama Ukurasa wa Pili na yale majibizano na msichana anayemtaka, yatakufanya usiishie tu kucheka bali ujiulize ‘hivi huyu jamaa aliwaza nini? Alikuja kudhihirisha kuwa yupo mbele ya wakati tena na kupigia mstari uwezo wa style kwa wimbo wake Baba Style uliojaa ufanisi wa hali ya juu kiuandishi. Sikiliza verse yake kwenye wimbo ‘Chochote Popote’ alioshirikishwa na K-Lynn. Na pengine Noorah aliamua kukomesha kabisa pale alipoalikwa na Mwana FA kwenye Unanitega. Kwa mara nyingine tena wawili hao walikuwa mbele ya wakati. Ujuzi wa mitindo na ubunifu wa mawazo katika nyimbo zake uliendelea kudhihirika kwenye ngoma zake zingine ukiwemo Lugha Gongana ulioanzisha ukaribu wake na B’Hits. Hapo palizaliwa pia ngoma ambayo bahati mbaya haikufanya vizuri sana lakini kama ukiweza kuisikiliza leo utagundua kuwa ilikutanisha rappers wawili wenye style moto kuwahi kutokea. Chambervernment iliwakutanisha Ngwair na Noorah na mdundo ukasimamiwa na Pancho Latino. Kwangu mimi hiyo ni moja ya ngoma kali zaidi za rappers wawili wanaojibizana baada ya Ingekuwa Vipi ya Mwana FA na Jay Moe. Sasa swali na msingi ni kama Noorah alikuwa mbele ya wakati, wakati sasa umefika mbona tunajifanya hatumkumbuki? Kama game linavyowafanyia pioneers wengi wa Bongo Flava, ndivyo Noorah anafanyiwa pia. Katika kipindi hiki ambacho walau sasa nyimbo zake zimefika katika wakati wake, Noorah alipaswa kuwa mmoja wa rappers ambao si tu wanasikika na kuzungumziwa sana, bali pia wanaofanya show kila weekend. Miaka ya hivi karibuni rapper huyo alipitia majaribu mengi ikiwa pamoja na kufanyiwa upasuaji mkubwa uliomfanya arudi kwao Shinyanga, kufiwa na aliyekuwa mke wake hadi kuwapoteza washkaji zake wa karibuni Ngwair na Mez B. ara ya mwisho namsikia Noorah bado alikuwa na uwezo mkali wa kurap na ambaye mtindo wake ungekuwa na biashara zaidi kwa sasa. Kama walivyo rappers wengine wa kitambo, alijaribu kuachia ngoma mbili tatu na zikaishia kuguswaguswa, kitu kilichomkatisha tamaa na kuamua kutulia kwanza kuusoma mchezo. Bado ninaamini kuwa Noorah ni msanii mkali na wakati wake wa ndio huu sasa japo kwa Tanzania kuishi mbele ya wakati wakati mwingine hugeuka kuwa mkosi badala ya kuwa baraka. SOURCE:BONGO 5

Saturday, February 14, 2015

Seck Baizo ft Mpenja & Stella-Sikuachi (Mix.Noiz)

Displaying SeckBaizo_500.png


Bofya HAPA http://goo.gl/sjcW1D  Kupakua wimbo wa Seck Baizo ft Mpenja & Stella ngoma ikiwa ni BongoFleva Category kwa jina "Sikuachi" kwa mahojiano/mawasiliano zaidi check na SECK BAIZO Kwa nambari +255 769 720 283 au +255 752 223 093 powered by www.vmgafrica.com #vmgafrica @noizmekah #supportafricanartists