- AZIMIO LA ARUSHA ilipitishwa na almashauri kuu ya TANU mwezi januari 1967 na kuthubitishwa na mkutano mkuu wa TANU mwezi marchi 1967 na kutolewa mwaezi februari 1967. IMANI YA TANU siasa ya TANU ni kujenga nchi ya ujamaa. misingi ya ujamaa imetajwa katika katiba ya tanu nayo ni
- kwamba binadamu wote ni sawa
- kwamba kila mtu anastahili heshima
- kwamba kila raia ni sehemu ya taifa na anayo haki ya kushiriki sawa na wengine katika serikali kuanzia ya mtaa mkoa hadi serikali kuu
- kwamba kila raia ana haki na uhuru wa kutoa mawazo yake,kwenda anakotaka .kuamini dini anayitakana kukutana na watu mradi havunji sheria
- kila mtu ana haki ya kupata kutoka kwenye jamii ifadhi ya maisha yake na mali yake aliyonayo kwa muhujibu wa sheria.
- kwamba kila mtu ana haki ya kupata malipo ya haki kutokana na kazi yake.
- kwamba raia wote kwa pamoja wanamiliki utajiri wa asili wa nchi hii ukiwa kama dhamana kwa kizazi chao.
- kwamba ili kuhakikisha uchumi wa nchi unakwenda sawa serikali lazima iwe na mamlaka kamili juu ya njia za muhimu kukuza uchumi.
- kwamba ni wajibu wa serikali ambayo ni watu wenye kuingilia kati kwa vitendo maisha ya uchumi ya taifa ili kuhakikisha ustawi wa raia wote na kuzuia mtu kunyonya kikundi kingine na kuzuia limbikizo la utajiri kufikia kiasi ambacho hakipatani na siasa ya watu wote kuwa sawa
- MADHUMUNI YA TANU:
- kwa hivyo basi ,makusudi na madhumuni ya TANU yalikuwa kama ifuatavyo...
- kudumisha uhuru wa nchi yetu na raia wake
- kuweka heshima ya mwanadamu kwa kufuata barabara kanuni za tangazo la ulimwengu la haki za binadamu
- kuhakikisha kwamba nchi yetu inatawaliwa na serikali ya watu wa kidemokrasia na ya kisoshalist
- kushirikaiana na vyama vyote vya siasa katika Afrika vinavyipigania uhuru wa bara lote la Afrika
- kuona kwamba serikali inatumia mali yote ya nchi kuondosha ujinga maradhi na umasikini
- kuona kwamba serikali inasaidia kwa vitendo kuunda na kudumisha vyama vya ushirika.
- kuona kwamba kila iwezekanapo serikali inashiriki katika hasa katika maendeleo ya uchumi wa nchi yetu
- kuona kwamba serikali inatoa nafasi sawa kwa wote wake na waume bila kujali rangi kabila wala dini
- kuona kwamba serikali inaondoa kila aina ya dhuluma vitisho ubaguzi rushwa na upotofu
- kuona kwamba serikali ya nchi yetu inasimamia barabara njia kuu za kuzalisha mali na inafuata barabar a siaisa ambayo inarahisisha njia ya kumiliki kwa jumla mali ya nchi yetu
- kuona kwamba serikali inashirikiana na dola nyingine katka Afrika kuleta umoja wa Afrika.
- kuona kwamba serikali inajitahidi kuleta amani na salama ulimenguni kwa njia ya chama cha umoja wa mataifa
- SIASA YA UJAMAA.>HAKUNA UNYONYAJI...nchi yenye ujamaa kamili ni nchi ya wafanya kazi,haina ubepari wala ukabila haina tabaka mbili za watu, tabaka la chini la watu wanaoishi kwa kufanya kazi,na tabaka la juu la watu wanaoishi kwa kufanyiwa kazi, na katika nchi ya ujamaa kamili mtu hanyonyi mtu bali hawezaye kufanya kazi hufanya kazi.nchi yetu ni ya wakulima na wafanyakazi lakini si nchi ya ujamaa kamili ina misingi ya ebepari na ukabaila wa vishawishi vyake.misingi hii ya ukabaila na upeapri yaweza ikapanuka na kuenea
- NJIA KUU ZA UCHUMI NI YA WAKULIMA NA WAFANYA KAZI.namna ya ya kujenga na kudumisha ujamaa ni kuthibitisha kuwa njia kuu zote za uchumi wa nchi yetu zinatawaliwa na wakulima na wafanya kazi wenyewe kwa kutumia vyombo vya serikali yao na ya vyama vyao vya ushirika, pia kuthibitisha kuwa chama kinachotawala ni cha wakulima na wafanyakzi. Njia kuu za uchumi ni kama arthi,misitu,madini,maji,mafuta na nguvu za umeme. Njia za habari,njia za usafirishaji,mabenki na bima,biashara za nchi za kigeni na biashara za jumla, <<<MAELEZO HAYA YATAENDELEA...
Home / AZIMIO LA ARUSHA
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)
Blogger Comment
Facebook Comment