Shinikizo rika ni hali ya mtu kufanya kitu kutokana na kikundi cha rika lake linalomzunguka au Mtu kupenda kitu kutokana na kuona kutoka kwa rika lake. Bahati si bahati ni kwamba mengi tunayoyaona siyo yale ya kusema ni vyema kuiga na kuleta manufaa kwetu kwa mfano matumizi ya madawa ya kulevya vijana wengi wamejiingiza kwenye matumizi kwasababu ya kuwaona watu flani wanatumia na bila hata kujua matokeo yake. Mahusiano ya kimapenzi yasio sahihi
matumizi ya madawa ya kulevya. kuacha masomo, nk ni mitihani ambayo vijana wengi hawajui maswali yake hata kujiuliza baada ya nini kinafata, kundi la vijana wanashauriana na kufanya kitu bila kujua matokeo yake na kwa wanafunzi huu ni mchanga wa moto bila viatu wengi wamepoteza masomo kwa kufukuzwa shule ama mimba zisizotarajiwa. Kijana kama wewe binafsi unatakiwa kujua mipaka yako na malengo yako binafsi bila kushawishiwa na mtu na hata ikitokea unashawishika ni ushauri hivyo unaweza kujua nini cha kufanya ili kutokatisha malengo yako. kuishi bila ratiba pia ni chanzo cha watu kuingia kwenye shinikizo la rika. Ni muda wa vijana kutambua kila wanachofanya kina matokeo gani na faida gani kwasababu mwisho wa shinikizo rika ni mzigo kwa familiya kwani yanapokuwa mabaya kila mtu huenda kwake. Mchuma janga hula na wa kwao kaa chonjo kijana maisha yako ni ndoto na mipango uliyopanga. - Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment