A TOWN BOYS ARUSHA

KARIBU SHULE YA MSINGI LORUVANI, KARIBU SANA NA JISKIE UPO NYUMBANI.

HAWALI YA YOTE NAOMBA NITAMBULISHE MAENEO NYETI KIJEOGRAFIA, MALIWATO AMA VYOO HIVI NDIYO SISI WANAFUNZI WA LORUVANI TUNATUMIA TUNAPOKUWA MASOMONI, SI UNAJUA MKULIMA HACHAGUI JEMBE SISI KITABU TU.
HIVI VYOO HUWA TUNAPANGA FOLENI KUVITUMIA SIUNAJUA LA KWANZA LA SABA WOTE KWA HAPO? MHH MASOMO NI MENGI UKIANZIA HAPA, CHOO CHA KULENGA FIZIKIA HIYO, MH KARIBU TENA SHULE YA MSINGI LORUVANI
HILI NI DARASA KWA MUONEKANO WA NJE, HUKO NDANI TUNASOMA MADAKTARI, WABUNGE,MARAISI,WASANII,MARUBANI NA WATU WA UWEZO TOFAUTI TOFAUTI, KWA MFANO MIMI KAKA MKUU NINA UWEZO SANA NA MAMBO YA KISAYANSI, MH KUNA RAFIKI YANGU NI MCHUNGUZI SANA NA JOGRAFIA ANAIWEZA,
DARASA KWA NDANI NI KAMA HIVI .KUNA MSEMO UNAOSEMA USIPOJIPENDA NANI ATAKUPENDA, BASI NAOMBA NIWAAMBIE SJAWAHI KUFIKIRIA KUHAMA LORUVANI, MH WAPI KAMA LORUVANI? SHULE HII ILIKUWEPO TANGU ENZI ZA MWALIMU NA BABA YANGU KASOMA NA SASA HIVI NI DAKTARI. SIWEZI KUHAMA LORUVANI NGOJA NIENDELEE KUKUONYESHA MADARASA YETU, KARIBU TENA
UBAO KWENYE DARASA NI KAMA CHAKULA MEZANI YAANI NDIYO MHUSIKA MKUU, HAPO NI UBAO UNAOTULISHA MAARIFA YA KUJENGA NCHI YETU YA UJAMAA, MADAWATI NAYO JAPO TUNAKAA KWA KUBANANA ILO NI SOMO PIA KWETU, ACHANA NA NYUMBA ZA BUIBUI UNAZOONA NA VUMBI VUMBI HIZO KWETU SIYO TABU KITABU KINASONGA MBELE.
NAPENDA KUTUMIA LUGHA NZURI NIKIZUNGUMZA KWAKUWA NIMESOMA LORUVANI NA NAJUA LUGHA NZURI HULETA MUHAFAKA MZURI, HATA WIMBO WETU WA SHULE UNAIMBA "SHULE YETU LORUVANI INADUMISHA HEKIMA NA UMOJA" MWISHO WA KUNUKUU, KARIBU BASI HATA SIKU MOJA UJE UONE TUNAVYOSOMA HUENDA UKAVUTIWA NA MAISHA YETU YA SHULE, KWA MFANO KAMA WEWE NI RAISI ALAFU UMESOMA NA UMEONA PICHA KWANI HUTA PENDA KUJA KWETU?
HAKUNA ULINZI WA KUTISHA GETI LETU NDIYO HILI HAPA TUNAFUNGA NA JIWE KWA HIYO UKIJA UNASOGEZA TU JIWE ALAFU UTAKUWA UMEFANIKIWA KUINGIA, MHHH NAHISI KAMA KENGELE YA MARASANI IMELIA SASA ACHA MIMI NIKAPIGE KITABU KWA AJILI YA TANZANIA YANGU, UKIPENDA KUONA MENGI ZAIDI INGIA KATIKA MAKALA ZA JAMII KWENYE www.ulimwenguwavipaji.blogspot.com
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments: