A TOWN BOYS ARUSHA

KWANINI UNAHITAJI MTAJI MKUBWA KUANZA BIASHARA?..

MJASIRIAMALI, UJASIRI NA MALI,  MIPANGO YA KIJASIRI YA KUPATA MALI,
ujasiri umetajwa awali ya yote katika neno UJASIRIAMALI kwamba cha kwanza ni jinsi gani wewe ni jasiri wa kufanya mambo ambayo matokeo yake ni makubwa kwa upande chanya ama hasi, kuna faida na hasara pia hayo yote yanahitaji ujasiri kutenda. ujasiri ni mkubwa kama neno lenyewe kuna baadhi ya watu wameshindwa kujua hapa ujasiri kwenye mali upoje? umeshindwa kuwa mjasiri wa kufanya kidogo unataka vikubwa, kwa mfano mtu anaweza kukuambia anataka kuwa mfanyabiashara lakini hakuna anachokifanya juu ya msemo wake. Au baadhi ya watu wanakuwa na mawazo ya kibiashara ambayo yanahitaji mitaji mikubwa ambayo ni kama ndoto kutokana na maisha anayoishi na kipato chake.
Vijana wengi sasa hivi wanamapendekezo waliyobuni wanahitaji watu wa kuwapa mitaji au mwongozo fulani ila tatizo ni mapendekezo yao kuwa ni ya bajeti kubwa hadi kupelekea wao kushindwa kutokana na wingi wa fedha au kutoonekana kuanza kwa chochote yeye binafsi. wapo wakina mama wanahitaji mikopo ya kufanyia biashara uzuri wa bahati ni kupata nafasi na upande mwingine hawana elimu juu ya kuwa mjasiri na kupata mali mwisho wanakuwa wakiishi kwa kulipa madeni ya waliowakopesha. Anza leo kuwa mjasiri ili kesho upate mali acha kuwaza mitaji mikubwa wakati mawazo yako siyo makubwa kama biashara unayotaka kufanya, amini chini ndiyo mwanzo wa juu na basi kama upo chini hakuna upande mwingine kama siyo juu. Usiishi kiupotofu kwa kuogopa kutokuwa na pesa baki na neno la ukweli kichwani mwako kwamba ukubwa ulianzia udogoni. FIKIRI JUU YA KIDOGO ULICHONACHO KWANI NDIYO CHA CHAKO KIKUBWA. www.ulimwenguwavipaji.blogspot.com
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment