A TOWN BOYS ARUSHA

MTO UMEKAUKA. AU WEWE UNAONA NINI? MTO UMEKAUKA HAUNA MAJI.

 www.ulimwenguwavipaji.blogspot.com HUU NI MTO ULIOKUWA UKIPITISHA MAJI HADI MUDA MWINGINE MAFURIKO, ILA SASA UNAONA MAFURIKO YA NYASI KAVU ZILIZODONDOSHWA NA MITI KUASHIRIA KAME YA ENEO HILI.

ELIMU YA KUTUNZA VYANZO VYA MAJI IMEKUWA IKITOLEWA KWA MUDA MREFU HADI SASA, NJIA ZA KUHIFADHI MAJI NA VYANZO VYAKE KILA MTU AKAJUA.NA SASA NI MUDA WA KUONA MATOKEO YA KUHIFADHI AMA KUTOHIFADHI VYANZO VYA MAJI. NI AIBU KWA MWANADAMU ALIYAPEWA AKILI KULALAMIKA HAKUNA MAJI MAHALI ALIPO KUTA KUNA MAJI AWALI. MITO SASA NDIYO MAHALI PA KUTUPA TAKATAKA NA KAMA UAMINI HILI NITAKULETEA BAADHI YA PICHA NA MAELEZO JUU YA MITO ILIYOGEUZWA JALALA NA BINADAMU TIMAMU, HATA KWA YOTE TUNAYONUFAIKA KUTOKA KWENYE MITO BADO HAKUNA ANAYEJALI UWEPO WA  MTO AU KUTOKUWEPO HUKU MAJI YAKIWA NI TATIZO SUGU. UKIONA MATOKEO HAYA  INATOSHA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA MAZINGIRA YETU TUNAYOISHI NDANI YAKE. MAHALI WANAPOISHI WANYAMA PORI NI PASAFI KULIKO WANAPOISHI WATU WENYE AKILI TIMAMU, CHUNGUZA AKILI YAKO NA MWENENDO WAKO JUU YA MAZINGIRA NA CHUKUA HATUA STAHIKI ZA KUBORESHA MAKAZI. KUWA WA KWANZA KUIFANYA DUNIA KUWA MAHALI PAZURI PAKUISHI.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment