A TOWN BOYS ARUSHA

KAMA AFRIKA ITAUNGANA ITAFANYA NINI KWA MUUNGANO HUO??.


UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI UDHAIFU, AFRIKA INAPOTAKA KUUNGANA INATAKA KUUNGANA NA NANI NA KUFANYA NINI....? NA NI NANI..? WANAOUNGANA AFRIKA VIONGOZI AU WANAOONGOZWA? WAAFRIKA WANAWEZA KUUNGANA VIONGOZI WAKATENGANA AU VIONGOZI WANAWEZA KUUNGANA WANAOONGOZWA WAKATENGANA? NI MASWALI MACHACHE TU YA KUJIULIZA UNAPOTAKA MUUNGANO WA AFRIKA. UMOJA WA NCHI ZA MASHARIKI MWA AFRIKA UMEKUJA NA TANZANIA NI NCHI MOJAWAPO NDANI YA HILI, TUNAUNGANA KUFANYA NINI AMBACHO TUMESHINDWA KUFANYA BILA KUUNGANA? NI VIONGOZI AU WANANCHI WAMEUNGANA? TANZANIA KUNA MUUNGANO TAYARI ILA AFYA YA MUUNGANO IKOJE? MUUNGANO HUU UNAWEZA KUISHI MIAKA 50 IJAYO? TANGANYIKA NA ZANZIBER NA SASA NI TANZANIA NA KENYA,UGANDA,RWANDA,BURUNDI UMOJA UNAKUJA PALIKOTENGANA AU WALIOTENGANA WANATAKA KUUNGANA? ALII MBA BOB MARLEY AFRIKA UNGANENI NA KUTOKA KWENYE UKANDAMIZAJI, UNYONYAJI NI SAWA ILA MNYONYAJI HUYO NI NANI? BADO NI KABURU AU MUAFRIKA MWENZAKO? NCHI NYINGI SASA NI MAANDAMANO NA MIGOMO HUKU SILAHA ZIKIPATA SOKO KUBWA. WAAFRIKA TUNAUNGANA KUPIGANA AU KUIJENGA AFRIKA YETU. MAMA AFRIKA MAMA MZAWA WA VIPAJI NA AKILI , MKIMBIZI ALIYEKIMBIZWA NYUMBANI KWAKE SABABU YA VITA, MAMA AFRIKA MAMA IMARA MAMA MZAWA RANGI NYEUSI, WEWE AFRIKA MAMA SHUJAA DHIDI YA UMASKINI MAGONJWA VITA NA NJAA, GODORO LA KULALIA BILA NYUMBA, MAHALI PA KUFIKIA BILA AMANI, WATOTO WA KULEA BILA MATIBABU, MUME WA KUKUOA BILA MAISHA, HAYO YOTE NI DHIDI YA MWANAMKE KUTOKA AFRIKA. MIMI MTOTO WA AFRIKA MIMI NDIYO MLINZI AMA ASKARI VITA, SINA ELIMU WALA FAMILIA, MIMI MPIGANAJI VITA, NATUMIA SILAHA ZA MOTO NA KUPIGANA NA WAAFRIKA WENZANGU, NAIPENDA AFRIKA NDOMANA NAIPIGANIA. HAYO NI JUU YA MTOTO WA AFRIKA. KABLA HUJAUNGANA NA JIRANI JIUNGANISHE NA AMANI KWANZA. KILA LA HERI MUUNGANO WA AFRIKA
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment