A TOWN BOYS ARUSHA

TAZAMA SINTOFAHAMU HII: KINGA HAITAKIWI JAPO MALARIA HAIKUBALIKI.

 MBELE YA MACHO YAKO NI VYANDARUA AMBAVYO SERIKALI IMEONA BORA IWAPATIE WANANCHI WAKE BURE ILI MALARIA IKOME, MIMI NILIVYOONA HIVI NIKAJIULIZA NI MALARIA HAIKUBALIKI TU AU HATA KINGA DHIDI YAKE HAITAKIWI? 
 KUNA WANAOTUMIA HIVI VYANDARUA KUTENGENEZA KAMBA ZA KUFUNGA MIFUGO, MABANDA YA KUKU, WATOTO KUCHEZEA,KUVULIA SAMAKI,KUZIBIA MATUNDU YA NYUMBA ZA KUISHI. KWANGU YOTE HAYO YANAMAANISHA KINGA HAITAKIWI JAPO MALARIA HAIKUBALIKI.
 KAMA HIVI VYANDARUA NI MKOMBOZI JUU YA UGONJWA HUU BASI WATU HAWA WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA, KAMA HIVI VYANDARUA HAVIJAKIDHI VIWANGO BASI SI VIBAYA WAKIFUGIA KUKU NA VINGINE VINGI.
NAAMINI HAKUNA KINACHOTOKEA BILA SABABU, BASI WEWE UNAHISI SABABU ZIPI ZINAFANYA HAYA KUTOKEA, ULIMWENGU HUU WA VIPAJI UTAKULETEA MAHONI YA WANANCHI HAO ILA KWA SASA WEWE BASHIRI HALI HII. ALAFU WOTE TUSEME MALARIA HAIKUBALIKIIIIIIII.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment