A TOWN BOYS ARUSHA

ZITTO: UNAFUU WA PAYE HAUMSAIDII MFANYAKAZI

Dodoma. Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe amesema unafuu wa Kodi ya Mshahara (Paye), uliotangazwa na Serikali kwamba umeshuka kutoka asilimia 13 hadi 12 ni mdogo hautamsaidia mfanyakazi kubaki na fedha kwa ajili ya matumizi wala kujiwekea akiba.
Katika mchango wake wa maandishi kwa Bajeti ya Serikali jana, Zitto alisema ni dhahiri kuwa Paye ni chanzo kikubwa cha mapato ya ndani ya Serikali lakini akapendekeza kipunguzwe zaidi.
Mbunge huyo alishauri kiwango cha chini cha mshahara unaokatwa kodi kiwe Sh330,000 na kiwango cha chini cha kodi kiwe asilimia tisa.
“Kiwango hiki cha kodi pia kinawezekana kwa Serikali kuchukua hatua dhidi ya matumizi mabovu,” alisema Zitto na kuongeza:
“Kwa mfano, kwa mujibu wa Taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa ndani wa Serikali mwaka 2013, mfumo wa kukagua utumishi wa umma umegundua kuwa jumla ya wafanyakazi wa Serikali 6,500 walikuwa wameajiriwa mara mbili kwa majina yaleyale, 2,700 mara tatu na kulikuwa na watumishi 2,500 waliokuwa wanachukua mishahara miwili mpaka mitatu kila mwezi.”
Alisema hatua ya kuondoa matumizi mabovu kutokana na kulipa mishahara hewa pia inaweza kusaidia kupunguza mzigo wa kodi kwa wafanyakazi nchini.
“Serikali hutumia wastani wa Sh360 bilioni kila mwezi kulipa mishahara na kati ya hizo Sh10 bilioni zimekuwa zikilipwa kwa watumishi hewa,” alisema Zitto.
Alisema nafuu ya kodi kwa wafanyakazi nchini katika sekta zote na hasa wafanyakazi wa kima cha chini itachochea matumizi binafsi ya bidhaa na huduma na hivyo kuchangamsha uchumi na kuwezesha uwekaji wa akiba.
“Nashauri ukaguzi zaidi ufanyike katika utumishi wa umma ili kumaliza kabisa tatizo la wafanyakazi hewa.”
Aliipongeza Serikali kwa kuanzisha kodi ya zuio ya ada kwa wakurugenzi wa kampuni na mashirika akisema itaongeza mapato ya Serikali.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment