Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili
(Muhas), imeboresha hali ya vitendea kazi katika sehemu ambazo ni
hatarishi zaidi ili kulinda watendaji wake dhidi ya maambukizi ya vvu
yanayoweza kutokana na mazingira ya kazi
Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi
Duniani juzi, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Ephata Kaaya, alisema
miongoni mwa maeneo yaliyopewa kipaumbele zaidi ni kwenye maabara zote
sambamba na ufungaji wa mashine za kutoa kondomu za kiume kwenye mabweni
ya wanafunzi
“Sisi wa Muhimbili kutokana na elimu tunayojifunza
au kufundisha sio kweli kwamba tuko kwenye hali bora zaidi ya kuweza
kujikinga na ugonjwa wa Ukimwi ni lazima tuchukue tahadhari,” alisema
Kaaya.
Alisema zaidi ya asilimia 90 ya maambukizi yote ya
vvu nchini yanatokana na kujamiiana, huku asilimia iliyobaki ikiangukia
kwenye sababu nyingine za maambukizi
Makamu Mkuu wa chuo hicho alisisitiza kuwa ni
wajibu wa kila mmoja kuunganisha nguvu katika kupunguza maambukizi na
adha za kuugua Ukimwi kwani madhara yake yanafahamika kuanzia kwenye
familia, jumuiya na taifa na hayatofautiani kati ya jamii na jamii au
familia na familia
Kaaya alisema hadi sasa dunia imeshapoteza watu
takribani milioni 25 tangu kugundulika kwa kirusi cha vvu mwaka 1981,
huku wengine wapatao milioni 35 wakiishi na virusi hivyo
0 comments:
Post a Comment