A TOWN BOYS ARUSHA

MIMI NA WEWE TUITUNZE ARUSHA





www.ulimwenguwavipaji.glogspot.com.  Arusha kama inavyosifika ni mji wa kitalii na mahali pazuri kwa kila mtu kuishi.Haya ni baadhi ya maeneo pembezoni mwa Arusha karibu na Mlima Meru, ni maeneo mazuri kwa kutalii na kufurahi kutokana na hali ya hewa kutoka kwenye msitu mnene wa kijani pamoja na miinuko. Pia panapatikana maporomoko ya water falls maji yanayodondoka kutoka umbali wa futi kama 50 kutoka juu na ukiachna na maeneo ambayo ni mazuri kwa kutalii kuna jamii ya kabila la kimasai wanao ishi pembezoni mwa mlima na pori ilo watu ambao wamekuwa sehemu ya utalii. Kama unavyojua mahali wanapoishi viumbe vya aina yeyote panakuwa na mahitaji ya muhimu kama maji,chakula na makazi na hiki ndicho kilicholeta changamoto. Leo watu hawapiki bila kuni ambayo ni miti imekatwa, lazima kujenga kwa kukata miti ya kujengea na kukata miti  ili kupata mahali pa kujenga.msitu huu unaanza kupoteza yale ambayo tumeona sisi ila bado watoto na wajukuu wetu hawajakiona. Leo kuna watalii wa ndani wanaoenda kutalii kwa wingi na wanasaau kutunza kile wanachokitumia ni porini lakini utakutana na plastiki zikizurura.Ndugu Mtanzania wajibu wa kutunza mali yako ni wa kwako. mazingira ambayo ndo yanatupatia kila kitu leo hayajaliwi na sisi wanadamu wenye akili. Yatunze mazingira yakutunze na pamoja tudumishe utalii wa ndani kwa manufaa ya kizazi kijacho...KARIBU KUTEMBELEA MLIMA MERU NA MAENEO YAKE, KARIBU KUIJUA ARUSHA
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment