WASANII WA MAIGIZO KUTOKA SANAWARI NI CHANGAMOTO YA SIKU ZA USONI
www.ulimwenguwavipaji.blogspot.com. Hawa ni baadhi ya wasanii kutoka kundi la jamii ya sanaa sanawari walipokuwa katika ziara ya semina ya utunzaji wa mazingira walipotembelea baadhi ya maeneo ili kujionea ni kwa jinsi gani swala la mazingira linahitaji watu wa kutoa mbinu za kufanya mazingira yapendwe.Zaidi ya maigizo pia tunaitazama jamii yetu inapata nini kutoka kwetu wasanii na ndo mana tumeamua kuanza na mazingira kama sehemu ya kujali afya ya kila mmoja wetu....hayo ni baadhi ya maneno yaliyosemwa na mmoja wa wasanii hao na kusema kuwa wanajiandaa kuzindua kampeni ya mazingira ambayo itakuwa na jina ambalo ni kama adhabu kwa wasio tunza mazingira na hivyo mda ukifika itatambulishwa rasmi na pia itahusisha shule za sekondari na msingi katika kuimiza upandaji wa miti.na kutotupa taka ovyo.Sisi kama jamii ya sanaa tunaamini kuwa jamii itajivunia sanaa yetu kwa mengi. JAMII YA SANAA....NI SISI WANASANAAAAAAAAA
0 comments:
Post a Comment