A TOWN BOYS ARUSHA

"WAPOKEENI WAGENI MAANA MTAPOKEA MALAIKA BILA KUJUA" HII NI RISALA KWAKO MGENI RASMI WA ULIMWENGU WA VIPAJI.BLOGSPOT,

 NGUGU MGENI RASMI, HUU NI ULIMWENGU WA WATU WENYE VIPAJI, KARIBU SANA KARIBU SANA...NAOMBA NIANZE KUKUELEZA YALE TULIYO YAFANYA NA BAADAE YALE TULIYOPANGA KUYAFANYA, SISI ULIMWENGU WA VIPAJI HUU UKIWA MUUNGANIKO WA WATU WATATU WENYE VIPAJI NA LENGO LA KUINUA VIPAJI VYA WENGINE, MWAKA 2009 TULIANZA RASMI KUTANGAZA VIPAJI VYETU AMBAVYO TUMEZALIWA NAVYO. TULISHIRIKIANA BILA KULIPWA NA MTU NA KUANZISHA VIKUNDI VYA VIJANA AMBAVYO VILIKUWA NA WATU WENYE UWEZO NA VIPAJI,A. TOWN BOYS ARUSHA MUZIKI  KIKUNDI CHA HIP HOP NA JAMII YA SANAA KWA MAIGIZO, SARAKASI, KUCHORA KUCHEZA MUZIKI. 
 NDUGU MGENI RASMI, TUMEHUSISHA IDADI TOFAUTI YA VIJANA NA KWAMBA MAFANIKIO PIA YANALENGA IDADI KUBWA YA VIJANA WENYE VIPAJI, TULIANDAA MAPENDEKEZO YETU NA KUYAFIKISHA KWA WATU WENYE UWEZO WA KIFEDHA NA HATA KIONGOZI WA KISERIKALI LAKINI HATUKUFANIKIWA TULICHOPENDEKEZA, HATUKURUDI NYUMA BADO TULIAMINI KATIKA TUNACHOFANYA. ILIFIKA TUKAONA TUFANYE BILA MSAADA WOWOTE NA HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA...
 MGENI RASMI, TULIKUMBANA NA CHANGAMOTO AMBAZO SISI TUNAZIITA NJIA YA USHINDI, VIFAA KATIKA HILI NI JAMBO NAMBA MOJA, TULIANDAA MATAMASHA YA MTAANI KWAAJILI YA KUWAONYESHA JAMII ILIYOTUZUNGUKA KWAMBA TUNAWEZA NA TUNAHITAJI KUSONGA MBELE. TUKAJIKUSANYA NA KUPATA VYOMBO VYA KUANZIA KWA GHARAMA ZETU WENYEWE ILA UDUNI WA VYOMBO ULITUKWAMISHA. SIXTEEN RECORDS NI STUDIO YA MUZIKI NA MMOJA WETU AKIWA NDIYE PROJUZA( ERICK TEMU, RICK"S FITTY} NI STUDIO ILIYO REKODI NYIMBO ZETU ZOTE KABLA HATUJAKUTANA NA CHANGAMOTO YA STUDIO KUUNGUA VIFAA VYOTE NA KUANZA UPYA, TULIFANYA MATAMASHA SITA TU NA KUKWAMA KUTOKANA NA HALI YA UCHUMI KWAKUWA HATUINGIZI KIPATO KUPITIA VIPAJI ILA TUKIAMNI HAKUNA CHA KUTULIPA VIZURI ZAIDI YA HIVI VIPAJI
 TULIFANYA AMBAYO KILA MTU ALIPENDA KIENDELEE, VIPAJI VIDOGO VIKAJITOKEZA NA KUONEKANA, WATU KUJUA WANA VIPAJI PIA NI MAFANIKIO TULIYOJIVUNIA KWA WAKATI MGUMU KAMA HUU SWALA LA KUWAPATA WATU WA KUTAZAMA VIPAJI VYETU LILIKUWA WAZO LETU KUU, KWA KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII, KWA KUPITIA BLOG HII, KWA KUPITIA KWETU TULIPENDA KUONGEZA IDADI YA WATU WANAOJUA TUNA VIPAJI. 
TUKIWA NA SPIKA MOJA, COMPUTA MOJA, KIPAZA SAUTI MOJA NA KWA MOYO MMOJA TULIANZA KAZI. BILA SISI KULIPWA, BILA KUPATA MAENEO MAALUM YA KUONYESHEA VIPAJI NA MDA MWINGINE TUKIWA NA NJAA NA KIU TULIFANYA MATAMASHA KWA KILA JUMAPILI KWA KUTUMIA ENEO LA SOKO SANAWARI. TUKAWAPA WATU NAFASI YA KUONYESHA VIPAJI KWA DARAJA LA MTAA.
 MGENI ULIYE RASMI KWETU, TUNAAMINI KATIKA VIPAJI TULIVYOJALIWA NDOMANA TUNAFANYA KWA MOYO WA KUJITUMA TUNAAMINI NJIA YA KUFANIKIWA NI KUWA NA FIKRA SAWA PAMOJA NA KUJITUMA. HATUTEGEMEI KUACHA HIKI TUNACHOKIFANYA LEO WALA KESHO TUNA NDOTO ZA KUSHINDA UKUBWA WA MILIMA NA TUNA VIPAJI ZAIDI YA WATU WANAVYOFIKIRI AU KUONA KWA WEPESI.WAKATI TUNAANDAA MAPENDEKEZO HATUKUWA NA HATA CHOMBO KIMOJA NA BILA MTU WA PEMBENI YEYOTE KUTUINUA TUMEFANIKIWA KUWA NA KOMPUTA PAMOJA NA SPIKA AMBAZO NI NDOGO MNO KWA KUWEZA KUKIDHI HAJA YETU.
"WAPOKEENI WAGENI MAANA MTAPOKEA MALAIKA BILA NYIE KUJUA" TUNATANGAZA KUKUPOKEA LEO, KESHO NA SIKU ZOTE, USIONE HATARI KUTUMIA MDA WAKO KUJUA KUHUSU SISI KARIBU KWETU SANAWARI KARIBU ULIMWENGU WA VIPAJI SHIRIKIANA NASISI KUINUA VIPAJI KWA CHOCHOTE KILE AMBACHO MOYO WAKO UNAKUTUMA NA KWA JINA LA MUNGU UKABARIKIWE SIKU ZOTE. WAJULISHE JAMAA NA RAFIKI KUHUSU SISI WAJULISHE KWAMBA KUNA ULIMWENGU WA VIPAJI ARUSHA SANAWARI. AHSANTE NA KARIBU TENA.  
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment